Polisi yaonya magari ya serikali, ambulance yanayovunja sheria

Jeshi la polisi Kanda Maalum Lazaro Mabosasa 

Muktasari:

Amesema wanaoongoza kuvunja sheria ni magari ya serikali 

Dar es Salaam. Jeshi la polisi Kanda Maalum limepiga marufuku magari ya serikali, magari ya vyombo vya ulinzi na usalama na yale ya wagonjwa kupita kwenye barabara zisizoruhusiwa kwa kuwa sio matumizi salama.

Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mabosasa ametoa marufuku hiyo leo Juni 14  ikiwa ni siku tatu baada ya gari la wagonjwa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuligonga lori na kusababisha vifo vya watu wa wanne wakiwamo wanafunzi wawili  wa chuo hicho.

Amesema wanaoongoza kuvunja sheria ni magari ya serikali ambayo hupita barabara za magari yaendayo kasi na zile zilizokatazwa kupita.

"Barabara imetengwa kwa ajili ya magari yaendayo kasi matokeo yake wanaleta vurugu na wengine kusababisha ajali" amesema Mambosasa.

Amesema jeshi hilo litaendesha msako mkali na yeyote atakayekamatwa, sheria itafuata mkondo wake.