Adakwa na polisi kwa kujifanya polisi, daktari

Tuesday July 23 2019

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto leo Julai 23, 2019 akionyesha vazi la kidaktari alilokuwa akilitumia Rajabu Kambi ( 23 ) mkazi wa Area A Jijini hapa ( aliyeshika picha)  ambaye  pia alikamatwa na sare ya jeshi la polisi (jangle green), pistol ya bandia na hoster yake picha yake akiwa amevalia sare za JWTZ ambapo vyote alikuwa anavitumia kwa utapeli. 

By Rachel Chibwete, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Rajabu Kambi (23) kwa madai ya utapeli na kujifanya daktari na askari polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 23, 2019 kamanda wa polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema kijana huyo pia amekutwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

“Kwa kuwa alikuwa akivaa sare hizo za polisi walimuamini. Waliotapeliwa ni wapangaji na wenye nyumba, madereva bodaboda waliokuwa wakimpakia kwenye pikipiki na kumzungusha maeneo mbalimbali kisha hawalipi fedha yoyote.”

“Muda wote anakuwa amevaa kofia ngumu kwa sababu alikuwa bado hajapata kofia (ya polisi) na wananchi walimuamini wakidhani ni askari kweli,” amesema Muroto.

Muroto amesema mbali na kushona sare hizo za polisi, kijana huyo alikuwa na bastola bandia na kuna wakati akikuwa akijifanya daktari katika hospitali mbalimbali na kuwatapeli wagonjwa kwa madai atawasaidia kutoa wito kwa hospitali husika wachunguzwe vizuri afya zao.

Amesema watu wenye tabia kama za kijana huyo wanahatarisha usalama wa wagonjwa na kuleta picha mbaya wa hospitali husika.

Advertisement

Muroto amesema polisi pia wanamshikilia Mussa Pungu kwa tuhuma za kukutwa na  kete 132 za dawa ya kulevya  aina ya heroin.

Advertisement