Balozi: Mikopo ya kilimo changamoto kwa wajasiriamali

Balozi wa Denmark nchini Einar Jensen akipokea zawadi kutoka kwa Dk Anna Temu msimamizi wa mradi wa kuwaongoezea ubunifu wajasiriamali wa Ushirika wa wajasiriamali wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sugeco). Picha na Kalunde Jamal

Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen amesema wajasiriamali wa sekta ya kilimo wanapata changamoto ya mikopo kutokana na matunda ya uwekezaji katika sekta ya kilimo kuchukua muda mrefu kuzaa matunda.

Akizungumza wakati wa kufungua kampuni za Ushirika wa wahitimu wajasiriamali wa Chuo Kikuu Sokoine (Sugeco) , Jensen alisema  kuna haja ya kuwapo msukumo wa kufanya tafiti, uvumbuzi, ubunifu ili kuyaongezea mazao thamani.

“Kama hakuna ubunifu na uvumbuzi wa vitu vipya, mazao yatakuwa hayana thamani na kuendelea kuwatesa wajasiriamali walioamua kuzitumia fursa zilizopo katika kilimo, ”alisema Jensen.