Advertisement

Chadema kujadili ushauri wa wazee Maalim Seif kuwania urais

Uongozi wa Chadema umesema utaanza kujadili ushauri wa baraza la wazee la chama hicho, kuhusu kumvuta Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif kuwania urais kupitia Chadema.

Katibu Mkuu wa Chadema Vicent Mashinji 

BY Hussein Issa, Mwananchi hissa@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Baraza la Wazee la Chadema jana walishauri Maalim Seif kuhamia Chadema na kuwania urais.

Advertisement

Dar es Salaam.Uongozi wa Chadema umesema utaanza kujadili ushauri wa baraza la wazee la chama hicho, kuhusu kumvuta Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif kuwania urais kupitia Chadema.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 12, Katibu Mkuu wa Chadema Vicent Mashinji amesema ni muhimu kufuata ushauri na kuufanyia kazi.

“Wale ni wazee walitoa maoni yao hivyo chama kitajadili na kutoa tamko,"amesema.

Jana Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema, Hashimu Juma alisema  CUF ikipasuka Zanzibar, Chadema wanachukua nafasi na kumkaribisha Maalim Seif na wabunge wake Chadema.

"Lengo la upinzani ni kuhakikisha maendeleo yanakuwepo nchini hivyo kwa kuwa CUF ipo katika mgogoro Seif anaweza kuhamia Chadema kwenye nafasi ileile na atapata nafasi ya kuwania urais,"alisema Juma.

 Soma Zaidi: VIDEO: Chadema yamtaka Maalim Seif

More From Mwananchi
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept