Chagueni viongozi wenye shughuli za kufanya- Kadutu

Muktasari:

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyikia kata ya Kashishi wilayani Kaliua mkoani Tabora, Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu alisema wapo wanachama wasiokuwa na shughuli na endapo watachaguliwa watakuwa mzigo na wasumbufu.

Wakati wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakisema hawako tayari kupangiwa safu ya viongozi, mbunge amewataka kuchangua wenye shughuli za kufanya badala ya wanaoshinda vijiweni.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyikia kata ya Kashishi wilayani Kaliua mkoani Tabora, Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu alisema wapo wanachama wasiokuwa na shughuli na endapo watachaguliwa watakuwa mzigo na wasumbufu.

“Wapo baadhi ya wanachama wanaowagawa viongozi na wenzao kwa kuwa na majungu, wanategemea kupata chochote kutoka kwa viongozi jambo ambalo halikubaliki,” alisema Kadutu.

Awali, baadhi ya wakazi wa kata hiyo walimweleza mbunge huyo kuwa hawatakuwa tayari kupangiwa safu ya uongozi kwa kuwa wana akili za kutambua kiongozi asiyekuwa na makandokando.

“Huu si wakati wa kuchaguliwa viongozi kwa kuwa ikiwa hivyo ina maana wametudharau,” alisema Magida Sasi.