VIDEO: Dk Bashiru atinga UDSM

Katibu Mkuu Mteule wa CCM Dk Dk Bashiru Ally akizungumza na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk Rasul Ahmed Minja  alipowasili chuoni hapo.

Muktasari:

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amestaafu juzi.


Dar es Salaam. Katibu Mkuu Mteule wa CCM, Dk Bashiru Ali amewasili katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alikokuwa akifundisha.

Dk Bashiru ameonekana leo Mei 30, katika chuo hicho, akisalimiana na kupongezwa na wahadhiri wenzake pamoja na wanafunzi, ikiwa ni siku moja baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

Dk Bashiru ametuliwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM, kushika nafasi hiyo, akimrithi Abdulahman Kinana.

Awali baada ya kiongozi huyo kufika chuoni aliingia katika jengo la Utawala na baadaye kuelekea Idara ya Sayansi ya Sanaa na Utawala alikokuwa akifanyia kazi.

Akiwa kwenye idara hiyo, Dk Bashiru alizungumza na Mkuu wa Idara hiyo, Rasul Ahmed Minja ambaye pia alimlaki kwa shangwe na kumpongeza kwa uteuzi.