Dk Tizeba ataka uzalishaji zaidi mbegu za maharage

Wednesday June 20 2018
pic tizeb

Arusha. Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amewaagiza watafiti wa kilimo cha mbegu mpya za maharage kuongeza uzalishaji ili mbegu hizo ziwafikie wakulima kwa wingi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 20, 2018 wakati akizungumza katika uzinduzi wa mbegu bora za maharage katika kituo cha utafiti wa kilimo cha Selian (SARI) kilichopo mjini hapa.

Amesema kwa sasa kazi ya utafiti imekwisha, hivyo wanatakiwa kuzalisha kwa wingi mbegu hizo ili ziweze kuwafikia wakulima wengi zaidi mwakani.

“Mfanye hivyo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuhamia kwenye mbegu mpya za uzalishaji wa mazao,” amesema.

Advertisement