Dk Tulia amtaja Ruge kuanzisha Tulia Trust

Muktasari:

Naibu Spika amesema kwa mara ya kwanza kukutana na Ruge ni wakati akianzisha tamasha lake la  ngoma za asili la Tulia Trust.


Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema asilimia kubwa ya mawazo ya kuanzishwa kwa taasisi ya Tulia Trust, ni ya Ruge Mutahaba.

Dk Tulia ameyasema hayo leo Jumatano Februari 26, 2016 alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Redio Clouds.

Amesema ni mtu aliyekuwa akiwapa moyo vijana na kutaka watu wanaomlilia kuondoka kwake,  ni vyema waishi katika maneno yake.

 “Mimi nilipitia maisha ya kuuza mchicha, maandazi, naamini Ruge angekuwepo kipindi  kile kuna mawazo ambayo ningeweza kuyachota, nimepokea msiba wake kwa shukrani na huzuni kwa kuwa ni mtu ambaye alikuwa na mchango kubwa kwa watu wengi.

“Ni mtu ambaye ulikuwa unampigia simu na kumuomba mawazo yake, hivyo unafikiria leo mtu kama huyo hayupo, unawaza namna ya kutafuta rafiki mwingine wa aina yake,” amesema Dk Tulia.