Idadi ya maiti ajali ya MV Nyerere yaongezeka

What you need to know:

Miili zaidi ya watu waliokufa kwenye ajali ya kivuko cha Mv  Nyerere imeendelea kuopolewa name sasa idadi ya maiti imefikia 225.

Ukara. Miili ya watu iliyoopolewa katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere imefikia 225 baada ya saba kupatikana leo Septemba 23, 2018.

 

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema leo asubuhi Septemba 23.

Amesema wanaendelea kutoa taarifa zaidi za upatikanaji miili hiyo kadiri inavyipatukana.

 

Anasema baadhi ya maiti zilizokuwa zimezama chini ya maji, zimeanza kuibuka na kuelea na tangu alfajiri miili minne imeonekana na kuopolewa katika fukwe za Bwisya.

 

Amesema uchimbaji wa makuburi unaendelea kwa ajili ya maziko ya miili ambayo haijatambuliwa.

Makaburi hayo yanachimbwa hatua zaidi ya 250 kutoka gati la Bwisya ambako shughuli za uokoaji zinaendelea.

 

Akizungumzia mazishi hayo, Mongella amesema wapo marehemu waliotambuliwa na ndugu zao lakini wakaomba wazikwe katika utaratibu ulioandaliwa na Serikali.

 

"Wanaotambua na kuwa tayari kuchukua miili ya ndugu zao kwa maziko ya kifamilia wanaruhusiwa. Serikali inatoa ubani wa Sh500, 000 kwa kila maiti inayotambuliwa na kuchukuliwa," amesema Mongella