Kaliua vijiji vinakuwa kwa kasi

Wednesday August 14 2019

Mkuu wa wilaya ya Kaliua, Abel

Mkuu wa wilaya ya Kaliua, Abel Busalama,kushoto,akiwa na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi,Angelina Mabula.picha na Robert Kakwesi. 

By Robert Kakwesi, Mwananchi [email protected]

Tabora. Wilaya ya Kaliua imesema mpaka sasa imepima viwanja 1,597 ambavyo bado vinaonekana kuwa vichache vikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa vijiji wilayani humo.

Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula ambaye yupo katika ziara mkoani Tabora, leo Jumatano, Agosti 14, 2019, Mkuu wa Wilaya hiyo, Abel Busalama amesema vijiji vinakuwa kwa kasi huku vingine vikianza kuungana kama Usinge na Ugansa vyenye watu zaidi ya 50,000.

Amesema kunahitajika kasi ya upimaji viwanja na wilaya imeweka mkakati wa kutumia wapimaji binafsi ili kuharakisha kazi ya upimaji.

Busalama amebainisha kwamba kasi ya ukuaji mji na vijiji wilayani Kaliua, ni kubwa na kwamba, kunahitajika usimamizi mzuri kudhibiti ujenzi holela.

Kuhusu migogoro ya ardhi, Busalama amesema kuna migogoro 69 ambayo bado inashughulikia katika wilaya za .

Advertisement