Chura apatiwa mchumba Julieth

Saturday January 19 2019

 

La Paz, Bolivia. Romeo alichukuliwa miaka 10 iliyopita wakati wanabiolojia walipojua aina hiyo ya chura ilikuwa katika shida, lakini hakutarajiwa kubaki peke yake kwa muda mrefu.

Romeo, anayejulikana kama chura wa pekee ulimwenguni, ameishi miaka 10 ya kutengwa katika hifadhi ya Bolivia.

Wanasayansi wanasema wamempatia mchumba kwa jina Juliet baada ya safari ya kwenda msitu wa Bolivia.

Chura watano wa majini walipatikana katika vidimbwi vya maji na kukamatwa, kwa kusudi la kuzalishana na kupandikiza upya wanyama hao kwenye pori.

Teresa Camacho Badani, ni mkuu wa kitengo cha viumbe hai katika hifadhi asili iliyopo Cochabamba na kiongozi wa safari hiyo.

Anatarajia kwamba vyura hao wa jinsia tofauti watapaendana. "Romeo ni mtulivu na hana mizunguko," aliiambia BBC na kuongeza: "Romeo ana afya na anapenda kula lakini ana aibu na mpole."

Hata hivyo, Juliet ana utu tofauti sana: "Yeye ana nguvu sana, huogelea na anakula sana, wakati mwingine anajaribu kutoroka."

Vyura watano - wanaume watatu na wanawake wawili - ni vyura wa kwanza wa maji kuonekana katika pori kwa miaka kumi, licha ya utafutaji uliofanyika katika jangwa la Bolivia.

Alivutia hisia za mataifa mwaka mmoja uliopita juu ya kutafuta kwake mwenzi, na hata alipewa kurasa katika mtandao wa kutafuta mpenzi.

Vyura waliopatikana hivi karibuni walitengwa  katika hifadhi ya makumbusho, ambapo huko wanapambana kuhakikisha viumbe hao wanabaki hai.

Chris Jordan kutoka Shirika la Hifadhi la Wanyama pori ulimwenguni anasema kuna hatari ya kuwaweka wanyama kama mateka.

Hata hivyo kuna vyura wachache  porini ambao wanaweza kulinda idadi yao kwa mda mrefu.

"Tuna nafasi halisi ya kuokoa chura wa maji - kurejesha sehemu ya kipekee ya uhai wa misitu ya Bolivia, na kuzalisha taarifa muhimu juu ya jinsi ya kurejesha aina sawa ya vyura hao katika hatari kubwa ya kutoweka."

Advertisement