Mtafiti aliyezuia HIV kwa watoto tumboni achunguzwa

Tuesday January 22 2019

 

Beijing. Mtafiti ambaye alidai kutengeneza watoto waliozaliwa kijenetiki, anakabiliwa na uchunguzi wa polisi wa China, vyombo vya serikali vilisema jana huku mamlaka zikithibitisha kuwa mwanamke wa pili alipata mimba wakati wa majaribio.
He Jiankui aliishtua jamii ya wanasayansi mwaka jana baada ya kutangaza kuwa amefanikiwa kubadilisha jeni za mapacha wa kike waliozaliwa Novemba, kuwazuia wasiambukizwe Virusi vya Ukimwi (HIV).
Aliuambia mkutano uliofanyika Hong Kong kwamba kuna "uwezekano wa mimba nyingine" ya wapenzi wengine wa pili.
Uchunguzi wa serikali umethibitisha kuwepo kwa mzazi mwingine na kwamba mwanamke husika bado ni mjamzito, shirika la habari la China, Xinhua.
Mama huyo mtarajiwa na watoto wake pacha wa kike kutoka katika uja uzito wa kwanza, watawekwa chini ya uangalizi wa madaktari, mchunguzi aliiambia Xinhua.
Uchunguzi wa serikali ya Hong Kong ulibaini kuwa "alighushi nyaraka za naadili" na "kwa makusudi alikwepa kuwa chini ya usimamizi," kwa mujibu wa Xinhua.
Aliandaa timu ya mpango huo huo bila ya kuhusisha mtu na timu hiyo ilihusisha wafanyakazi kutoka nje ya nchi na kutumia teknolojia ambayo "haina uhakika wa usalama wala ufanisi" ili kufanya isivyo halali marekebisho ya kiinitete (embryo), ilisema.
Wachunguzi waliiambia Xinhua kwamba mwanasayansi huyo alikuwa akitafuta umaarufu binafsi na kutumia fedha alizotafuta mwenyewe kufanya jaribio hilo lenye utata.
Wapenzi nane waliojitolea --wanaume walio na HIV na wanawake ambao hawakuwa na HIV -- waliridhia mpango huop kwa kusaini makubaliano, lakini wapenzi wawili kati yao wakajitoa baadaye.

Advertisement