VIDEO: Achomwa moto kwa kuiarifu polisi tukio la kutaka kubakwa

Muktasari:

  • Licha ya hayo, Aprili 6 siku 11 baada ya unyanyasaji huo unaodaiwa, Nusrat alikwenda shuleni kwake kufanya mitihani yake ya mwisho

Dhaka, Bangladesh. Msichana mmoja Nusrat Jahan Rafi amemwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto shuleni kwake katika mji Dhaka kitongoji cha Feni nchini Bangladesh baada ya kutoa taarifa polisi za kunyanyaswa kingono na mkuu wake wa shule.

Akiwa kituo cha polisi mjini humo, Nusrat alieleza mashtaka. Alitakiwa kupewa mazingira salama ili aweze kutathmini yaliyomtokea. Badala yake alichukuliwa video na ofisa wa polisi husika kupitia simu yake huku akielezea yaliyompata.

Katika video hiyo Nusrat anaonekana wazi akiwa na mkanganyiko huku akijaribu kuficha uso wake kwa mikono.

Polisi anasikika akisema malalamiko hayo siyo ya msingi huku akimlazimisha Nusrat atoe mikono usoni. Baadaye video hiyo ilivifikia vyombo vya habari nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa rafiki zake, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka juu ya paa la shule kwa ajili ya kumficha.

Hata hivyo wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu watano, waliokuwa wamefunika uso walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi hiyo alipokataa wakammwagia mafuta ya taa na kumchoma moto.

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi, Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa "walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe. Mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada ya kutoroka eneo la tukio. Aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa.

"Nilijaribu kumchukua dada yangu shuleni na kujaribu kuingia shuleni, lakini nikazuiwa, sikuruhusiwa kuingia," alisema kaka yake Nusrat , Mahmudul Hasan Noman.

"Nisingezuiwa, jambo kama hili lisingemtokea dada yangu," alisema