Ajeruhiwa kwa risasi msikitini

Monday August 12 2019

Olso, Norway. Mtu mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi akiwa msikitini katika kitongoji cha Oslo mjini Baerum, Norway.

Polisi nchini Norway wamedhibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Agosti 12 wakati mtu huyo alipokuwa katika ibada ya siku kuu ya Eid.

Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo alikamatwa kabla hajaleta madhara zaidi.

Mkurugenzi wa msikiti huo, Irfan Mushtaq alikiambia kituo cha televisheni cha TV2 kuwa mtuhumiwa huyo aliingia katika msikiti huo akiwa ameshika silaha mbili ambazo ni bunduki na bastola.

Mushataq alisema mtuhumiwa huyo alivunja mlango wa vioo kabla ya kuanza kufyatua risasi ovyo na kumpata muumini huyo.

“Mmoja wa washiriki wetu alipigwa risasi na mtu mweupe aliyevaa kofia ya pikipiki pamoja na sare,” alisisitiza Mushtaq.

Advertisement

Advertisement