Amenasa uwanja wa ndege tangu mwaka jana

Muktasari:

  • Hati aliyopewa ya kusafiria na Israeli ikaisha muda wake alipokuwa njiani katika uwanja wa kimataifa wa Bole, Ethiopia baada ya Niger kumkataa tena. Mpaka wa leo bado amenasa hapo

Addis Ababa,Ethiopia.Israel, Raia mmoja wa Niger ambaye amefukuzwa nchini Israeli amenasa uwanja wa ndege nchini Ethiopia tangu  Novemba mwaka jana.

Raia huyo Eissa Muhammad, 24, amenasa kwenye kiwanja hicho jijini Addis Ababa baada ya nchi yake kugoma kumpokea.

Akizungumza na Shirika la Habari la BBC, alisema kwamba "Nimekuwa nikikaa hapa (uwanja wa ndege) katika mazingira magumu, hakuna kitu, hakuna kitu kabisa..."

Kijana huyo alifukuzwa Israel baada ya kubainika kwamba akiishi Israeli bila ya kibali alihamia nchini humo akitokea  Niger mwaka 2011, akiwa na miaka 16 ili kutafuta maisha.

Anasema aliwalipa wasafirishaji wa binaadamu ili kumpitisha nchini Libya na Misri kabla ya kuingia Israeli kwa miguu.

Alipofika jijini Tel Aviv, Tel Aviv, Muhamad aliishi kwa kutegemea kazi duni kwenye majumba ya kuishi wanafunzi na kiwanda cha kuzalisha pipi.

Baada ya kushikiliwa  kwa zaidi ya miezi sita, Israeli ilimpatia hati ya dharura ya kusafiri na kumpakia kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia kuelekea Niger kupitia Addis Ababa Novemba.

Hata hivyo, baada ya kuwasili Niamey, mji mkuu wa Niger, alishikwa na maofisa wa uhamiaji  wakidai kuwa hati yake ya kusafiria ilikuwa ni ya kughushi.

"Hawakunitaka kuingia Niger. Hawakunikubali kabisa," amesema Muhamad.

"Walinifunga mikono na miguu yangu na kunilazimisha kuingia kwenye ndege na kunirudisha Niger ambapo walinikataa tena."