Boris ‘akacha’ mdahalo wa kampeni Uingereza

Muktasari:

Mdahalo huo ulandaliwa na Kituo cha Televisheni cha Sky

Washington, Marekani. Mgombea wa kiti cha Waziri Mkuu nchini Uingereza, Jeremy Hunt amemtupia lawama mpinzani wake Boris Johnson kuwa anakwepa kushiriki midahalo ya ana kwa ana kuhusu hatma ya mchakato wa Brexit.

Hunt, ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza alisema hayo leo June 24, kuwa uamuzi wa mpinzani Boris hauna afya katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai.

“Uamuzi wa Boris wa kuepuka fursa ya kushiriki mdahalo ulioandaliwa na kituo cha Televisheni cha Sky ni kitendo cha kukosa heshima,” alisisitiza Hunt.

Hunt alisema raia wa Uingereza wanahitaji kufahamu na kupatiwa majibu juu ya kile wagombea hao watafanya iwapo mmoja wao atachaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala Conservative na hatimaye uwaziri mkuu.

Hata hivyo, Boris ambaye ameng’aa katika duru zote tano za awali za uchagz huo, amedai yeye ndiyo mshindi wa nafasi hiyo kwa kuwa ni mgombea pekee anayeweza kukamilisha mchakato wa Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ifikapo Oktoba 31.

Jumla ya wagombea 17 walijitokez kumrithi Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ambaye alitangaza kujiuzulu baada ya kushindwa kuitoa nchi hiyo katika Umojoja wa Mataifa.

Hata hivyo, ni wagombe wawili pekee ambao wamebaki katika kinyang’anyiro hiko ambao watapigiwa kura na wajumbe wa baraza zima la chama cha Conservative linalotarajiwa kukutana Julai, mwaka huu.