British Airways yapoteza mwelekeo, abiria wachanganyikiwa

Monday March 25 2019

London, Uingereza. Abiria wa Shirika la Ndege la Uingereza British Airways wameonesha kushtushwa baada ya kupanda ndege iliyokusudiwa kwenda jijini Dusseldorf, Ujerumani badala yake ilienda kutua Edinburgh, Scotland.

Ndege hiyo aina ya BA3271 ilianza kuondoka uwanja wa ndege wa jijini London saa 1:47 asubuhi na ilitakiwa iende Ujerumani Mashariki.

Hata hivyo, rubani aliyekuwa anaiongoza ndege hiyo alipatiwa mpango wa safari uliomwelekeza kwenda katika mji mkuu wa Scotland na aliweza kufanikiwa kutua jijini humo saa tatu kamili asubuhi.

Baadhi ya abiria walitumia mtandao wa kijamii wa Twitter wakielezea kukasirishwa kwao na tangazo hilo la ndege kubadili mwelekeo ghafla.

Mmoja wa abiria aliyejitambulisha kwa jina la Son Tran, aliuliza  ni kwanini ndege ielekekee mji wa Edinburgh badala ya Dusseldorf.

Msemaji wa uongozi wa uwanja wa ndege alisema kwamba  wanafanya kazi  kuhakikisha wanapata majibu ya nini kilichotokea

Advertisement