Congo kujenga mradi wa umeme mkubwa zaidi dunia

Sunday August 11 2019

Congo. Serikali ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza mchakato wa ujenzi wa mradi mkubwa wa kituo cha uzalishaji umeme wa Grand Inga III

Kituo hicho kinatazamiwa kuzalisha megawati 40,000 za umeme kitagharimu dola bilioni 14 karibu Sh31 trilioni kitasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii.

Mradi huo ambao unatarajiwa kujengwa kwa ufadhili wa nchi ya China unaaminika utakuwa wa kwanza kwa ukubwa duniani. Kwa sasa mradi wa bwawa la Gorges III la nchini China ndiyo kubwa zaidi duniani inayotoa megawati 22,500.

Kwa sasa nchi ya Congo inategemea vyanzo viwili vya uzalishaji wa umeme vilivyojengwa katika Mto Congo zaidi ya miongo mitatu iliyopita vya Inga I na Inga II.

Kwa mujibu wa Serikali ya Congo, ujenzi wa mradi huo ukikamilika utatoa unafuu na kupunguza uhaba wa umeme ambao kwa sasa ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya nchi hiyo na bara la Afrika.

"Mradi huu ni wa kipekee, kwa sasa hakuna sehemu yoyote duniani unaweza kupata kiasi kikubwa cha umeme kama hapa,” alisema mhandisi na kampuni ya umeme ya Taifa nchini Congo, Omer Kawende.

Advertisement

Oktoba mwaka jana, Rais Joseph Kabila alisaini makubaliano na vikundi viwili vya wawekezaji wa China na Uhispania ambao pamoja na mambo mengine walijitolea kufadhili masomo ya ufundi kabla ya kujenga kwa mradi huo.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia (WB), asilimia 19 pekee ya wananchi wa Congo ndiyo wanapata huduma ya umeme kwa sasa.

Macho yote sasa yamo mrithi wa Kabila, Felix Tshisekedi, aliyeapa kuungana nusu ya idadi ya watu kwenye gridi ya taifa katika kipindi cha muongo mmoja. Inga III, washauri wake wanasema, ni moja ya vipaumbele vyake - hata kama Tshisekedi hajathibitisha atashikamana na muungano wa Uhispania na Wachina, ambao bado hawajapewa mkataba wa makubaliano.

Advertisement