Daktari atumia mbegu zake za kiume kuzalisha watoto 49

Muktasari:

Imekuwa ni kawaida kwa daktari huyo kutumia mbegu zake kupata watoto badala ya za wateja wake

Totterdam,Uholanzi. Mahakama moja nchini Uholanzi imeidhinisha ombi la familia zinazotaka vipimo vya vinasaba DNA vichukuliwe dhidi ya mmiliki wa kliniki ya uzazi ya daktari anayeshutumiwa kutumia mbegu zake za kiume kuzalisha wanawake.

Jan Karbaat anashukiwa kuwa baba wa watoto  49 katika kituo cha afya alichokimiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.

Vipimo sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake  Aprili, akiwa na umri wa miaka 89.

Wakili wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

Jan Karbaat alijiita "muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa".

Kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati kulikuwa na taarifa kwamba alidaiwa kughushi data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiume na kuzidisha idadi inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za uzazi.

Katika kesi ya mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba kuna kesi zinazojumuisha  mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wake ambaye anasura inayofanana na daktari.

Taarifa za vinasaba DNA zitabakia  kuwa siri hadi pale watoto watakapoonyesha kuwa kuna sababu za kuamini daktari alikuwa baba yao.

Hatimaya, kama taarifa za vinasaba-DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya 1980 kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba hawangepaswa kuwepo.

Joey, ambaye anaamini Jan Karbaat huenda ni baba yake ameiambia BBC: " Ina maana kubwa kwangu ... Tunatumai kupata majibu ."

Wakili wa familia ya Karbaat anapinga kufanyika kwa vipimo vyovyote vya vinasaba DNA.

Wakati wa uhai wake, daktari mwenyewe alikataa kufanya vipimo hivyo.

Hata hivyo, mwezi uliopita,kijana wake Jan Karbaat alitoa vinasaba vyake DNA vipimwe ambavyo vilionyesha kuwa daktari anaweza kuwa babawa watoto 19, waliozaliwa kwa njia ya uzazi wa kutungishwa mbegu kwa lugha ya kitaaamu IVF, kwa mujibu wa  ripoti ya shirika la habari la AFP.