Ethiopia yasitisha safari za ndege za Boeing 737 Max

Monday March 11 2019

 

Ethiopia. Shirika la Ndege la Ethiopia limetangaza kusitisha safari za ndege zake zote za Boeing 737 Max 8 kuanzia jana Machi 10 hadi taarifa zaidi itakapotolewa.

Shirika hilo limeendelea kusema kwamba licha ya kuwa chanzo cha ajali hakijajulikana, wameamua kuchukua hatua hiyo kama tahadhari ya ziada.

Paia mkaguzi wa safari za ndege China ameagiza kampuni zote za ndege nchini China kusitisha safari za ndege aina hiyo  ambayo ni ya muundo sawa.

Advertisement