Filamu ya mpango wa kumng'oa Clinton kwa kashfa ya Monica Lewinsky yaiva

Muktasari:

Kashfa hiyo ilimuhusisha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Bila Clinton ambaye alituhumiwa kufanya ngono na mfanyakazi wa Ikulu na nusu isababishe ang'olewe madarakani.

 

Monica Lewinsky atatayarisha mfululizo wa vipindi vya uhalifu kuhusu mchakato wa kumuondoa rais wa Marekani, Bill Clinton ambazo zitaanza kurushwa hewani wiki chache kabla yha uchaguzi wa mwaka 2020, kituo cha FX kilisema jana Jumanne.

Msimu wa tatu wa vipindi hivyo vya "American Crime Story (Hadithi ya Uhalifu Marekani), ACS" utanogesha matukio yaliyosababisha Lewnsky, mfanyakazi wa Ikulu ya Mareani, pamoja na wenzake wawili walivyojikuta wameingia katika "mchakato wa kwanza wa kumuengua rais wa nchi (ya Marekani) kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja," inasema taarifa ya FX.

Makala hiyo inakuja baada ya mbili za msimu wa kwanza za ACS ambazo zilihusu kesi ya mchezaji wa mpira wa miguu aina ya Kimarekani, O.J. Simpson na mauaji ya mbunifu maarufu wa mavazi, Gianni Versace.

Kutangazwa kwa msimu wa tatu kuliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakisema kuibuliwa upya kwa kashfa hiyo ya ngono ambayo nusura imuondoe rais kutoka chama cha Democratic madarakani, kutamnufaisha rais aliyeko madarakani kutoka chama cha Republican, Donald Trump.

Wakati huohuo, uamuzi wa Democratic kuunga mkono harakati ya kumuondoa Trump madarakani unazidi kuwa imara, huku zaidi ya nusu ya wabunge wake wakikubaliana na mchakato huo, kwa mujibu wa tafiti za vyombo vya habari.

"Watu watapendelea sana hili (makala za mchakato wa kumuengua rais) wakati wa uchaguzi wa rais na itakuwa kitu kipinndi kizuri," alisema John Landgraf, kiongozi wa FX, alipozungumza na wachambuzi wa televisheni waliokutana Los Angeles.

"Siamini kama (vipindi hivi) vitaamua nani atakuwa rais wa Marekani," alisema akijibu moja ya maswali.

Lewinsky alisema katika taarifa yake kwa Vanity Fair kuwa awali hakupenda kujiunga na mradi huo, lakini baadaye akakubali ili ashike kikamilifu maelezo kuhusu kashfa hiyo.

"Nimefurahi kwa maendeleo tuliyofiki kama jamii ambao inaruhusu mtu kama mimi ambao kihistoria walinyamazishwa, kutoa sauti yao baadaye katika mazungumzo," alisema akirejea kampeniu kali ya #MeToo dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.

"Watu wenye nguvu, mara nyingi wanaume, hutumia walio chini yao kwa njia mbaya," alisema Lewinsky akisisitia kuwa "maelezo haya (katika vipindi hivyo) ni mazuri."

Wahusika wengine katika vipindi hivyo vilivyotayarishwa na Ryan Murphy ni Sarah Paulson anayeigiza kama Linda Tripp, ambaye alifichua siri kuwa Clinton alikuwa katika mapenzi na Lewinsky. Nafasi ya Lewinsky itaigizwa na Beanie Feldstein na Annaleigh Ashford ataigiza kama Paula Jones, ambaye alimshtaki Clinton kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Makala hizo zitazinduliwa Septemba 27 mwakani na uchaguzi wa Marekani utafanyika Novemba 3.