Gavana Sonko alegeza masharti ya usafiri

Tuesday December 4 2018

 

Nairobi, Kenya. Gavana wa Jiji la Nairobi, Mike Sonko amesitisha uamuzi wake wa kuzuia mabasi ya usafiri wa umma maarufu kama Matatu kufika katikati ya jiji baada ya utekelezaji wake Jumatatu kukumbwa na malalamiko.
Tamko la Sonko la kuondoa marufuku hiyo lilitolewa Jumanne alfajiri likisema “nimesitisha kuanzia sasa" kuruhusu kufanyika mazungumzo na “pande zilizoathirika” ili kupata suluhu ya msongamano katikati ya jiji.
Sonko katika taarifa hiyo alisema, alipata mrejesho wa mateso waliyopata abiria, wamiliki wa Matatu, wafanyakazi na wafanyabiashara waliopata usumbufu mkubwa.
Alitangaza kusitishwa kwa tangazo Na 4479 lililowekwa kwenye Gazeti la Serikali Mei 12, 2017 majira ya saa 11.42 alfajiri kupitia Facebook alipozungumza mubashara kutoka ukumbi wa City Hall, makao makuu wa Halmashauri ya Kaunti ya Nairobi.

Ilivyokuwa
Marufuku iliyoondolewa ilikuwa inahusu utekelezaji wa sheria iliyoandaliwa na mamlaka za jiji la Nairobi kupiga marufuku magari ya usafiri wa umma maarufu kama matatu kuingia katikati ya jiji kuanzia Jumatatu.
Hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka, ililenga kupunguza msongamano wa magari. Sheria hiyo mpya ilianza kutekelezwa mapema alfajiri ya Jumatatu huku maofisa wa usalama barabarani wa kaunti ya Nairobi wakiwa wamejipanga kuzuia matatu kuingia sehemu ya katikati ya jiji.
Makali ya marufuku hiyo yalianza kuonekana asubuhi baada ya makumi kwa mamia ya watu walioachwa nje ya jiji kutembea kwa miguu kuelekea kazini au sehemu za biashara katikati ya mji huku polisi wakilinda maeneo muhimu ya kuingilia.
Baadhi ya maofisa waliokuwa wamejihami kwa silaha za moto walipelekwa katika vituo vipya vilivyowekwa nje ya jiji
Maofisa hao waliweka vizuizi vya barabarani katika eneo la Muthurwa, barabara ya Murang'a, Fig Tree A, barabra ya Desai, barabra ya Ngara, Hakati, Railways na kituo kikuu cha mabasi katikati ya jiji.
Amri yao kwa wahudumu wa matatu ilikuwa wazi: "Simama! Hakuna kuendesha gari kupita

Advertisement