Iran yadai shambulizi la mtandao la Marekani halikufanikiwa

Muktasari:

Nchi hiyo imedai kwa mwaka mmoja pekee imeweza kuzima majaribio milioni 33 ya mashambulio mtandaoni

Iran. Waziri wa Mawasiliano wa Iran, Mohammad Javad Azari amesema kuwa mashambulio ya mtandao yaliyofanywa na Marekani dhidi ya mifumo yake ya komputa inayotumika kufyatua makombora hayakufanikiwa.

Kupitia ukurasa wa Twitter, waziri huyo wa Iran aliandika leo June 24, kuwa Marekani ilijaribu kwa nguvu kubwa kuishambulia mifumo ya kompyuta zinazoongoza mifumo ya ulinzi ya Iran lakini jaribio hilo lilishindikana.

“Mwaka uliopita tulifanikiwa kuzima majaribio milioni 33 ya mashambulio mtandaoni,” alisisitiza waziri Azari.

Hata hivyo, waziri Azari alisema mashambulizi hayo dhidi ya ni ugaidi.

Jumapili iliyopita, vyombo vya habari nchin Marekani viliripoti kuwa nchi hiyo ilifanya mashambulizi ya mtandao dhidi ya mifumo ya makombora ya Ira.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuachana na mashambulizi ya anga katika nchi hiyo yenye lengo la kulipiza kisasi.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi mawili yaliyofanywa na Iran ikiwamo lile la kuteketezwa kwa meli ya mafuta kwenye Ghuba ya Oman.

Jumanne iliyopita Iran iliitungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kwa madai kuwa ilipita katika anga lake jambo ambalo lilipingwa na Rais Trump na kudai kuwa ilikuwa katika anga la kimataifa.

Gazeti la Washinton Post liliandika kwamba, nchi hiyo liharibu mifumo ya kompyuta inayodhibiti roketi na mitambo ya kurushia makombora ya Iran.

Mvutano kati ya mataifa hayo mawili ulijitokeza tangu Marekani ilipojiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na kuiwekea vikwazo vilivyotikisa uchumi wa Iran.