Jela maisha kwa waraka ‘feki’ wa kigaidi

Muktasari:

  • Alikuwa akishinikiza mpenzi wake wa nje ya ndoa aliyekuwa akifanya kazi ya uhudumu wa ndege kuacha kazi na kwenda kuishi naye

New Delh, India. Mahama kuu nchini India imemuhukumu kifungo cha maisha jela mfanyabishara Birju Salla baada ya kuweka waraka feki kwenye choo cha ndege ya kampuni ya India-Jet Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka New Delhi kuelekea Mumbai.

Mahakama hiyo pia imemuamuru mfanyabishara huyo kulipa faini ya rupia milioni 50 karibu Dola za Marekeni 720,725.

Birju ambaye ni raia wa India katika utetezi wake alidai alitegemea ndege hiyo ingefunga safari zake na hivyo mpenzi wake angeacha kazi ya uhudumu katika kampuni hiyo na kuishi nae mjini Mumbai.

Hata hivyo, taarifa zaidi zinasema kuwa mfanyabishara huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake na muhudumu huyo.

Mfanyabiashara huyo alikiri kuwa aliandika waraka huo wa tishio la ugaidi na kuuchapisha katika ofisi yake kabla ya kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya safari yake Oktoba, 2017.

Waraka huo ulisema kuwa watekaji 12 na milipuko kadhaa ilikuwa ndani na kuamrisha ndege hiyo ielekezwe kwenye jimbo la Pakistan linalodhibitiwa na Wataleban la Kashmir.

Hata hivyo, Salla alikamatwa baada ya ndege hiyo kutua kwa dharura katika jimbo la Ahmedabad ikiw ani maili 483 kutoka Mumbai.

 

 

 

Salla ndiye mtu wa kwanza kushtakiwa nchini humo chini ya sheria mpya ya India zinazozuia utekaji nyara.

Awali Salla aliripotiwa kuwa alimuomba mpenzi wake ahamie Mumbai lakini alikataa na aliamini kwamba kwa waraka huo angeichafulia sifa kampuni hiyo ya ndege hivyo mpenzi wake kupoteza kazi na kuishi nae.

Afisa uhunguzi wa tukio hilo ameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba japo Salla hakufanya utekaji wowote kitendo alichokifanya kinamtia hatiani kwa kosa kujaribu kuiteka ndege kwa mujibu wa sheria ya India.

Mahahama hiyo imeamuru marubani wa ndege hiyo kupata mgawo wa Rupia 100,000 kila mmoja kutoka kwenye fidia atakayoitoa kwa mfanyabishara huyo kutokana na mkanganyiko walioupata, wahudumu wa ndege wao watapata Rupia 50,000 huku wasafiri watalipwa 25,000.

Hata hivyo, wakili wa mfanyabishara huyo, Rohit Verma, alisema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.