Kamera za CCTV zathibitisha mwandishi akiingia basi

Tuesday October 9 2018

 

Ankara, Uturuki. Picha za kamera za CCTV zinamwonyesha mwandishi wa habari raia wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi akiingia kwenye jengo la ubalozi mdogo wa nchi hiyo ulioko Istanbul na tangu hapo hajaonekana akitoka.
Jamal Khashoggi, 59, mkoaji mkubwa wa utawala wa Saudi Arabia aliingia kwenye ubalozi mdogo wa nchi hiyo Oktoba 2 ili kupata nyaraka kwa ajili ya harusi yake, lakini hakuonekana akitoka, na polisi wanaamini “aliteswa na kukatwa vipande vipande” ndani ya jengo hilo.
Picha hizo za CCTV zinamwonyesha Khashoggi akiingia langoni muda wa saa 7.15 mchana, Jumanne ya wiki iliyopita.
Mpenzi wake Hatice Cengiz, 36, anasema hajaweza kumwona tena akitoka licha ya kukaa nje kumsubiri hadi ubalozi huo mdogo ulipofunga shughuli zake siku hiyo.
Picha za CCTV ambazo gazeti la Washington Post limepata zinaonyesha dakika za mwisho ambapo Khashoggi alionekana akiwa hai ni wakati alipokuwa anatembea kuingia ndani ya ubalozi huo mdogo jijini Istanbul Jumanne.
Akizungumza na The Post, Cengiz anasema anahofia maisha yake katika mkesho wa kutoweka kwa mpenzi wake. Alisema alisubiri nje kwa saa kadhaa na mwishowe maofisa usalama walimwambia “hakuna mtu yeyote ndani” pale alipoulizia kuhusu mahali alipo mpenzi wake.
Ubalozi mdogo unasema mwanahabari huyo alitoka nje kwa kutumia mlango wa nyuma, japokuwa hakuna ushahidi wowote wa yeye kuwepo ndani ya jingo licha ya kamera za CCTV kuangaza eneo lote.
Serikali ya Saudi Arabia imekanusha vikali kufanyika kitu chochote kibaya ndani ya ubalozi huo na badala yake inasisitiza mwanahabari huyo aliondoka.

Advertisement