Kampuni zilizoagiza ndege za 737- Max 8 hizi hapa

Muktasari:

  • Kampuni za Marekani ndizo ambazo zinaonekana kuongoza kununua aina hiyo ya ndege

Washington, Marekani. Shirika la ndege la Southwest la nchini Marekani ndilo linaloongoza kwa kuagiza ndege za aina ya 737-MAX 8 na mpaka sasa wamenunua 31 na kuagiza zingine 280.

Mbali na shirika hilo, Flydubai la  Falme za kiarabu limenunua ndege 14 na kuagiza 237.

Aina hiyo ya ndege ndio iliyoanguka jana nchini Ethiopia ikiwa ni mali ya Shirika la Ethiopian Airlines ambayo pia iliua watu 157, wakiwa ni raia kutoka mataifa 35 duniani.

Mashirika mengine ni leli la Indonesia la Lion air ambalo mpaka sasa limeshanunua 14 ma kuagiza 187 huku kampuni ya Gecas iliyopo Marekani nao mpaka sasa wamenunua ndege hizo 22 na kuagiza 154.

Air lease ni shirika la usafiri ambalo lipo Marekani lenye makao makuu mjini Los Angels ambalo limenunua ndege  14 na kuagiza 154.

United airlines ya Marekani imeshanunua aina hiyo ya ndege 12 na kuagiza zingine 124 huku kampuni kubwa ya ndege inayofahamika kwa jina la Jet air ways yenye makao yake Mumbai, India ikiwa imeagiza ndege 125.