Kansela Ujerumani ashindwa kusimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa

Muktasari:

  • Mara kadhaa kiongozi huyo ameonekena hadharani akitetemeka akiwa katika hafla mbalimbali za kitaifa hali iliyozua wasiwasi juu ya afya yake.

Ujerumani. Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameonekana akiwa ameketi wakati wimbo wa Taifa hilo ukipigwa.

Hii ni mara ya pili katika muda wa wiki moja kwa Kansela huyo kuonekana akiwa ameketi wakati wimbo wa Taifa lake ukipigwa jambo ambalo si la kawaida.

Mara kadhaa kiongozi huyo ameonekena hadharani akitetemeka akiwa katika hafla mbalimbali za kitaifa hali iliyozua wasiwasi juu ya afya yake. Hata hivyo, Kansela huyo amesisitiza afya yake ni nzuri na hakuna haja ya kutia shaka.

Merkel aliyekuwa karibu na Waziri Mkuu wa Moldovia, Maia Sandu anayefanya ziara nchini humo alionekana akiwa amekaa wakati jeshi la nchi hiyo likitoa heshima mbele ya viongozi hao.

Wiki iliyopita Kansela huyo alionekana kuketi wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na waziri mkkuu wa Denmark.