Kazakhstan yapata rais mpya

Monday June 10 2019

 

Astana, Kazakhstan. Mrithi aliyeteuliwa moja kwa moja wa Rais wa zamani wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo.

Kassym-Jomart Tokayev ambaye ni mwanadiplomasia aliibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulikubwa na vurugu kati ya waandamanaji na polisi.

Tokayev alishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 70 ya kura huku kiongozi wa upinzani, Amirzhan Kossanov akipata asilimia 15 ya kura zote zilizopigwa.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kazakhstan, idadi ya wapigakura waliojitokeza kupigaji kura ni karibu asilimia 77 pekee.

Tokayev mwenye umri wa miaka 66, Machi mwaka huu alianza kukaimu nafasi ya urais baada ya Rais Nazarbayev ambaye aliiongoza nchi hiyo tangu Kazakhstan ilipopata uhuru wake kutoka kwa uliokuwa Muungano wa Kisovieti mwaka wa 1991 kujiuzulu.

Rais Nazarbayev ambaye anashikilia cheo rasmi cha kiongozi wa taifa, anatarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uendeshwaji wa siasa za kila siku kama kiongozi wa chama tawala cha Nur Otan

Advertisement

Advertisement