Kocha: Pacquiao anaweza kurudiana na Mayweather

Los Angeles, Marekani . Mwalimu wa ngumi, Freddie Roach alisema jana Jumatano kuwa anategemea Manny Pacquiao anaweza kupanga pambano la marudiano dhidi ya Floyd Mayweather baada ya gwiji huyo wa Phiollipines kuamua kupambana na Keith Thurman jijini Las Vegas mwezi huu.
Roach aliwaambia waandishi wa habari kuwa bado anakerwa na kipigo ambacho Pacquiao alipata kwa Mayweather katika pambano la mwaka 2015, ambalo lilitangazwa kama "Pambano la Karne" lakini likaishia kwa kukera mashabiki.
Baadaye Pacquiao alisema jeraha la bega alilokuwa nalo lilimzuia kupambana kwa kiwango chake katika pambano hilo la raundi 12, wakati Mayweather alitangaza kustaafu mwaka huo akiwa na rekodi ya kutoshindwa.
Pacquiao, ambaye alistaafu kwa muda mfupi mwaka 2016 na kurejea mwaka huohuo, ameendelea kupanda ulinzoni.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 atajaribu kutwaa ubingwa wa welterweight wa Chamacha Ngumi Duniani (WBA) Julai 20 atakapokabiliana na bondia wa Marekani, Keith Thurman, ambaye ni bingwa wa uzito huo na hajawahi kupoteza pambano, wakatapovaana kwenye ukumbi wa MGM Grand.
Roach, mwalimu w Pacquiao kwa muda mrefu ndani ya miongo miwili, anategemea kuwa ushindi dhidi ya Thurman unaweza kusafisha njia ya pambano la marudiano na Mayweather kama ataweza kumshawishi kurejea ulingoni.
"Tunatumaini tunaweza kumpata Mayweather mezani," Roach aliwaambia waandishi wa habari kwenye gym ya Wild Card jana Jumatano.
"Hatukufanya pambano kuwa kubwa siku ile (ya pambano la 2015). Bega la Manny halikumsaidia kabisa. Tangu wakati ule alifanyiwa upasuaji, sasa yuko vizuri kwa asilimia 100.
"Ningependa tupambane tena na Mayweather kwa sababu zikupenda jinsi tulivyopambana. Nilifadhaika."