Korea Kaskazini, Kusini zazidi kuweka kando tofauti zao

Friday September 14 2018

Seoul, Korea Kusini. Mataifa jirani ya Korea Kaskazini na Kusini yameamua kufungua ofisi ya kuratibu ushirikiano wao ndani ya Korea Kaskazini katika eneo la mpaka lenye ulinzi mkali wa kijeshi ili kurahisisha mawasiliano na kubadilishana taarifa kabla ya wakuu wa nchi hizo kukutana wiki ijayo jijini Pyongyang.
Ofisi hiyo iliyofunguliwa Ijumaa katika mji wa Kaesong ni sehemu ya hatua ya hivi karibuni ya mfululizo wa upatanishi kuwahi kuchukuliwa na Korea hizo mbili mwaka huu.
Ofisi hiyo ni ya kwanza ya aina yake tangu mataifa hayo mawili yagawanyike mwishoni mwa vita kuu ya pili ya dunia II mwaka 1945.
Wakorea kwa sasa wamekuwa wakiwasiliana kwa simu na faksi wanapotaka kupanga mazungumzo na kubadilishana taarifa. Lakini njia hizo mara kadhaa zimekuwa zikisitishwa kutokna na mgogoro unaohusu programu za silaha za nyuklia za Korea Kaskazini.
"Sasa tutaonana ana kwa ana, tutabadilishana mawazo haraka na kwa usahihi na kuweka vichwa vyetu pamoja kutatua matatizo yanayotusibu," alisema waziri wa muungano wa Korea Kusini, Cho Myoung-gyon wakati wa ufunguzi wa ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muungano wa Amani wa Korea Kaskazini, Ri Son Gwon alisema kwamba ofisi hiyo itawasaidia Wakorea kuwa na mazungumzo ya dhati na kuimarisha uhusiano wao.

Advertisement