Maafisa wa UN wauawa kwa bomu Libya

Sunday August 11 2019

Libya. Wafanyakazi watatu wa Umoja wa Mataifa (UN), wamefariki dunia baada ya gari lililobeba bomu kulipuka nje ya jengo la biashara la Arkan katika mji wa Benghazi ulio Mashariki mwa Libya.

Aidha, watu wengine tisa wamejeruhiwa katika tukio hilo wakiwamo wafanyakazi watatu wa Umoja huo.

Taarifa ya mlipuko huo imethibitishwa na msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric.

Taarifa zaidi zinasema mlipuko katika maduka ya Arkan ulitokea wakati watu walipokuwa wakifanya manunuzi siku moja kabla ya sikukuu ya Eid el- Hajj.

Kwa mujibu wabaraza la manispaa ya mji wa Benghazi, shambulio hilo liliwalenga wajumbe wa Umoja huo.

Shirika la habari la Ujerumani liliripoti kuwa, mlipuko huo umetokea jana Jumamosi Agosti 11, wakati pande mbili zinazohasimiana nchini humo zikiwa kwenye makubaliano ya kuweka chini silaha, pendekezo lililotolewa na Umoja huo.

Advertisement

Pendekezo hilo linakusudia kusimamisha mapigano katika mji mkuu Tripoli, wakati wa kusherehekea sikukuu ya Eid itakayoadhimishwa kesho Jumatatu.

Advertisement