Maandamano Sudan sasa yaelekea mahakamani

Monday March 4 2019

Khartoum, Sudan. Raia wanaompinga Rais wa Sudan, Omar al Bashir wameandamana kuelekea majengo ya mahakama katika miji tofauti nchini humo ikiwemo mji mkuu Khartoum.

Maandamano hayo ya jana yameitishwa na taasisi ya wataalam wa nchini Sudan iliyo kwenye mwavuli wa vyama huru vya wataalam nchini humo.

Vyama hivyo vinaongoza upinzani dhidi ya utawala wa Rais Al Bashir ambaye mwezi uliopita alitangaza hali ya hatari na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu isiyo na kibali na wakati huo huo polisi walipewa nguvu zaidi za kusambaratisha maandamano.

Hata hivyo hatua hizo hazijafanikiwa kuwazuia raia wa nchi hiyo kufanya maandamano yaliyochochewa na kupanda kwa bei za vyakula na uchumi uliodorora.

Advertisement