Mashabiki, wapinzani wa rais wa Taiwan watwangana nje ya hoteli aliyofikia Marekani

Friday July 12 2019

By AFP

Polisi jijini New York walilazimika kuamua ugomvi baina ya mashabiki na maadui wa rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen jana Alhamisi wakati akiwa ziarani nchini Marekani ambayo inaweza kuiudhi China.

Vyombo vya habari vya Taiwan zilirusha vurugu hizo zilizotokea nje ya hoteli ya Grand Hyatt, ambako Tsai anaishi wakati wa ziara yake nchini Marekani.

Wapinzani wa Tsai -- wengi wakiwa wanapunga bendera ya China -- walikuwa wakiimba na kupigana na mashabiki wake na mtu mmoja alionekana akikamatwa na kufungwa pingu.

Tsai atakuwa New York kwa siku mbli kabla ya ziara yake kwa nchi marafiki wa visiwa vya Caribbea.

Kwa kawaida, kiongozi wa nchi anayepita katika ardhi ya Marekani hatarajiwi kusababisha utata lakini kwa muda mrefu Taiwan imek=jikuta katika mazingira yasiyo ya kawaida ya kidiplomasia.

Kisiwa hicho cha kidemokrasia kimekuw ahuru kwa miongo saba lakini nchi nyingi hazikitambui kama nchi -- ikiwemo Marekani ambayo iliamua kutoitambua serikali hiyo ya Taipei na badala yake kuitambua China mwaka 1979.

Advertisement

Lakini Marekani imeendelea kuwa mshirika wake mkubwa na mtoaji wa silaha asiye rasmi.

China inaiona Taiwan kuwa ni sehemu yake na imepania siku moja kuiweka chini ya dola yake, na ikiwezekana kwa nguvu.

Inakorofishana na nchi yoyote ambayo inaisaidia Taiwan kidiplomasia.

Huku Marekani ikiwa katika mzozo mkubwa wa kibiashara na China kwa sasa, uhusiano wake na Taiwan umekua kwa haraka.

Advertisement