Mlipuko waua 73 Mexico

Sunday January 20 2019

 

Tlahuelilpan, Mexico. Idadi ya watu 21 waliofariki kutokana na mlipuko wa bomba la mafuta nchini Mexico yafikia 73, na wengine zaidi ya 70  wamejeruhiwa vibaya baada ya bomba la mafuta kulipuka na kushika moto nchini Mexico.
Inaaminika kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaodaiwa kuwa wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan, jimbo la Hidalgo.
Maofisa wanasema mamia ya watu walikuwa waking'angania kuchota mafuta kabla ya moto kuwaka ghafla.
Wezi wa mafuta, wanaofahamika kwa jina ‘huachicoleo’ wameongezeka katika baadhi ya jamii ya Wamexico.
Serikali imesema wizi huo uliligharimu taifa hilo takriban Dola 3 bilioni mwaka jana.
Rais Andrés Manuel López Obrador, ambaye aliingia madarakani  Desemba amezindua msako mkali dhidi ya wahalifu hao
Picha za televisheni zilionyesha moto mkubwa na watu walioungua  vibaya kutokana na moto huo.

Advertisement