Mlipuko waua 21 Mexico

Saturday January 19 2019

Tlahuelilpan, Mexico. Watu 21 wameuawa na wengine zaidi ya 71 wamejeruhiwa vibaya baada ya bomba la mafuta kulipuka na kushika moto nchini Mexico.

Inaaminika kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaodaiwa kuwa wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan, jimbo la Hidalgo.

Maofisa wanasema mamia ya watu walikuwa waking'angania kuchota mafuta kabla ya moto kuwaka ghafla.

Wezi wa mafuta, wanaofahamika kwa jina ‘huachicoleo’ wameongezeka katika baadhi ya jamii ya Wamexico.

Serikali imesema wizi huo uliligharimu taifa hilo takriban Dola 3 bilioni mwaka jana.

Rais Andrés Manuel López Obrador, ambaye aliingia madarakani  Desemba amezindua msako mkali dhidi ya wahalifu hao.

Advertisement