Mtendaji mkuu wa soka Australia ajiengua kuhofia Bodi ya Ligi

Thursday July 11 2019

By AFP

Sydney, Australia. Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Soka la Australia (FFA), David Gallop jana Alhamisi ametangaza kustaafu kazi mwishoni mwa mwaka wakati chombo hicho kinachoongoza mpira w amiguu kikifanya mageuzi yatakayozipa klabu sauti katika kuongoza mchezo huo.
Gallop, ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa miaka saba, amehusisha uamuzi wake na mpango wa mabadiliko hayo ambayo yatasababisha nafasi ya mtendaji mkuu kuondolewa.
Wiki iliyopita, timu iliyopewa nafasi ya kuangalia upya mfumo wa ligi za wachezaji wa kulipwa za Australia ilitangaza mapendekezo kadhaa ambayo yanaonyesha klabu zitakuwa na sauti kubwa zaidi katika uendeshaji wa mashindano makubwa.
Chini ya mapendekezo hayo, chombo kipya, ambayo kwa kiasi kikubwa kitaundwa na wawakilishi wa klabu, kitaendesha Ligi Kuu (A-League), Ligi ya Wanawake na ligi za vijana, wakati kikijiondoa kutoka chini ya mamlaka ya FFA.
Gallop alisema katika taarifa yake kuwa mapendekezo hayo yatasababisha mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa ligi za wachezaji wa kulipwa, na hivyo kufanya nafasi ya mtendaji mkuu wa FFA kuwa ndogo.
"Inaeleweka kwa kila mtu kuwa na muda wa kuamua waziwazi ni jinsi gani nafasi hiyo mpya itakuwa na uongozi mpya utakuwaje," alisema.
"Mpira wa miguu ni mchezo halisi na wananchi wengi wa Australia wenye historia tofauti wanataka kuuona ukikua na kuwa imara zaidi katika mmiongo inayokuja."
Januari, Gallop na FFA walijikuta katika shinikizo kubwa mwaka huu baada ya kutimuliwa kw autata kwa kocha wa wanawake, Alen Stajcic mwezi Januari, ikiwa ni miezi michache kabla ya fainali za Kombe la Dunia.

Advertisement