Mwanamke ‘aula’ Umoja wa Ulaya

Muktasari:

  • Ni Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Von der Leyen aliyechaguliwa kuwa rais wa Halmashauri Kuu EU

Brussels, Ubelgiji. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula von der Leyen amechaguliwa kuwa rais mpya wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya (EU).

Von der Leyen aliyedhibitishwa jana Jumanne Julai 16 na Bunge hilo alipata kura 323 kati ya 327 zilizopigwa na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa Leyen alisema “najihisi mwenye heshima na furaha. Kazi iliyoko mbele yangu inanifanya kuwa mnyenyekevu, ujumbe wangu kwenu nyote ni tushirikiane kwa kujenga.”

Rais Von der Leyen aliogeza kywa ajenda yake kuu ni kuwapo kwa usawa wa kijinsia ambako utawala wa sheria unaendelea kuheshimiwa.

"Nitahakikisha usawa kamili wa kijinsia katika timu yangu ya makamishna 28 wanaohitajika.”

Alisema takwimu zinaonyesha kwamba kati ya makamisha waliokuwapo wanawake ni asilimia 20 pekee jambo alidai kuwa siyo haki.

Mwanamke huyo mwenye nguvu ndani ya Ujerumani alisema pia changamoto iliyopo kwa sasa ni namna ya kuwa na dunia iliyo na afya.