Mwanamke amshona mdomo mwanaye

Wednesday June 5 2019

 

Naivasha, Kenya. Mwanamke mmoja mkazi wa mjini Naivasha, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya amemshona mdomo mtoto wake wa kiume baada ya kufanya vibaya katika masomo yake.

Gazeti la Daily Nation nchini Kenya limeripoti kuwa mama huyo alifanya tukio hilo jana Jumamosi June 4 nyumbani kwake Naivasha.

Akisimulia mkasa huo, mkazi mmoja wa Naivasha alisema  mwanamke huyo anayefanya kazi kwenye saluni ya urembo, aliumizwa na maendeleo ya mtoto wake huyo anayesoma darasa la tano.

“Ilianza kumpiga na mtoto akawa anapiga kelele ndipo alipoamua kumshona mdomo kwa kutumia sindano na uzi wa kushonea nguo,”alisisitiza.

Kwa mujibu wa jirani huyo, baada ya tukio hilo majirani waliingilia kati hata hivyo mtuhumiwa alikimbia.

Kamishna msaidizi wa kaunti hiyo, Julius Nyaga alidhibitisha kutokea kwa tukio akieleza kuwa ni kikatili .

Advertisement

''Polisi wanamtafuta mama wa mtoto baada ya uongozi wa shule kuripoti kwenye mamlaka,'' alisema Nyaga.

Kamishina huyo aliwataka wazazi kuacha kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto na badala yake kutafuta masaada wa kitaalamu ili kuwasaidia wanaopoona wanakwenda ndivyo sivyo.

Advertisement