Papa awajia juu wanasiasa

Saturday April 20 2019

 

Vatican.Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis  amewakemea wanasiasa wenye nyoyo ngumu na wanaopinga suala la uhamiaji.

Pia Papa amegusia unyanyasaji wanaofanyiwa watoto huku Kanisa Katoliki ilikiwa linaanza maadhimisho ya mwishoni mwa wiki ya sikukuu ya pasaka.

Papa ataongoza sala ya Pasaka leo usiku kabla ya ujumbe wake kwa ulimwengu wa Jumapili ya Pasaka.

Matamshi ya Papa ya Ijumaa Kuu, siku ambayo Wakiristo wanaamini Yesu alisulubiwa, yamekuja wakati ambapo bara la Ulaya limechukua msimamo mkali dhdi ya uhamiaji na kashfa za unyanyasaji wa kingono zimeshamiri katika kanisa lake la Katoliki.

Advertisement