Rais Trump alaani mauaji Marekani

Muktasari:

  • Jumapili iliyopita watu 30 walipoteza baada ya mtu asiyefahamika kuwafyatulia risasi watu waliokuwapo katika duka la jumla na mwengine kuvamia katika mji wa Dayton Oregon.

Washington, Marekani. Rais wa Marekani, Donald Trump amelaani mashambulizi yaliyofanywa katika duka la jumla la Walmart Texas mjini El Paso na Dayton Oregon Ohio.

Jumapili iliyopita watu 30 walipoteza baada ya mtu asiyefahamika kuwafyatulia risasi watu waliokuwapo katika duka hilo la jumla na mwengine kuvamia katika mji wa Dayton Oregon.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatatu Agosti 5 Rais Trump alisema kwamba chuki haina nafasi katika Taifa la Marekani na kwamba Serikali yake itahakikisha inalishughulikia suala hilo.

Katika hatua nyingine, Rais Trump alituma salamu za rambirambi kwa familia za waliouawa katika tukio hilo.

Aidha, Rais huyo wa Marekani alisema kwamba anaomboleza pamoja na waliofikwa na tukio hilo huko.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Jeshi la Polisi nchini humo linamshikilia mvulana mwenye umri wa miaka 21 kuhusika na tukio hilo.

Jeshi hilo lilisema kwamba mshukiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Patrick Crusius alikuwa akiishi katika eneo la Allen, Dalla Mashariki mwa El Paso.

Katika tukio la kwanza ilidaiwa kuwa mtu asiyefahamika aliyekuwa na bunduki kubwa aliwafyatuliwa risasi za moto watu waliokuwa ndani ya duka kubwa eneo la El Paso, Texas.

Ilidaiwa kuwa muda mfupi baadaye ilidaiwa mtu mwingine alishambulia katika mjini wa Dayton Oregon, Ohio na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.

Msemaji wa polisi wa El Paso, Robert Gomez alisema wakati wa tukio Texas Walmart likitokea kulikuwa na karibu wateja 3000 kwenye duka hilo.

Gomez alisema huenda shambulizi hilo lilichochewa na chuki za ubaguzi wa rangi na kuongeza kuwa mshambuliaji aliuawa katika eneo hilo baada ya kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi.

Hata hivyo, Gomez alisema kwa sasa mafisa wa polisi wanachunguza iwapo shambulio hilo ambalo lilifanyika maili chache kutoka mpaka wa Marekani na Mexico lilikuwa la uhalifu na chuki.

Gavana wa Jimbo la Texas, Greg Abbot amelitaja shambulio hilo kuwa ni mojawapo ya siku mbaya zaidi katika historia ya eneo hilo.

Kanda za video za CCTV zilizorushwa katika vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha mtu aliyevalia tishati nyeusi pamoja na vilinda masikio akifyatua risasi kwa watu waliokuwa dukani hapo.