Rais Trump atangaza hali ya hatari Marekani

Muktasari:

  • Kutokana na mvutano kati yake na Bunge kuhusu ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, Rais Donald Trump ametafuta namna ya kupata fedha zinazohitajika baada ya Bunge kugoma kuziidhinisha.

Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza hali ya hatari nchini mwake ukiwa ni mkakati wa kuhakikisha anafanikisha nia yake ya kujenga  ukuta mpakani na Mexico.

Tangazo hilo amelitoa leo, Februari 15 ili apate nafasi kutumia fedha za mfuko wa dharura na jeshi kufanikisha kujenga ukuta huo.

Ametangaza hatua hiyo baada ya Bunge la Congress mara kadhaa kugoma kutoa Dola 8 bilioni za Marekani zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa ukuta huo.

Hata hivyo chama cha upinzani cha Democratic kimesema kinakusudia kwenda mahakamani  haraka kupinga hataua hiyo ambayo kimeitafsiri kama matumizi mabaya ya madaraka.