Tani 167 za makolokolo zimezagaa mwezini

Thursday July 11 2019

By AFP

Washington, United States. Magari matatu, bendera sita za Marekani, na vyombo kadhaa vya uchunguzi vilivyofanikiwa kutua au kupata ajali, kamera. vifaa vingine na uchafu ni baadhi ya vifaa vilivyosalia mwezini ikiw ani matokeo ya uchunguzi wa anga.
Baadhi ya wataalamu wanapendekeza vifaa hivyo vipewe hadhi ya urithi ili kuvilinda dhidi ya shughuli za baadaye za watalii na za kibinadamu.
Yote hayo yalianza Septemba 13, 1959 wakati chombo cha uchunguzi cha Urusi, Luna 2 ilipoanguka kwenye bonde la Mare Imbrium.
Ilifuatiwa na safari kadhaa za uchunguzi mwezini, na baadaye ikawa zamu ya Wamarekani ambao walikwenda na programu za Ranger na Surveyor na baadaye, Julai 20, 1969, binadamu wa kwanza, Neil Armstrong na Buzz Aldrin walitua juu ya mwezi.
Wawili hao walitumia saa 22 kwenye "Bahari ya Utulivu (Sea of Tranquility)". Waliacha kila kitu ambacho hakikuwa muhimu kukirejesha duniani: kama kamera, viatu, vitu vya mwezini, vitu vya kumbukumbu
Safari nyingine tano zaidi za chombo aina ya Apollo ziliacha vitu vingine kibao.
Kwa hayo yote, mwezi una maeneo mengi ambay watu wameacha alama zao, kwa mujibu wa For All Moonkind, taasisi isiyo ya kibiashara ambayo nia yake ni kulinda urithi wa binadamu angani.
Vyote kwa pamoja vina uzito wa karibu tani 167.
"(Kisheria), maeneo hayo hayalindwi kabisa," alisema Michelle Hanlon, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mississippi ambaye alishiriki kuanzisha For All Moonkind mwaka 2017 baada ya kiongozi wa Wakala wa Anga wa Ulaya, Jan Worner kusema kwa utani kuwa anataka kuirejesha duniani bendera ya Marekani.
"Kwa hiyo viatu, magari na maeneo, ambayo ni muhimu kwa wachunguzi wa mambo ya kale, hayana ulinzi," alisema.
Hanlon anahofia kuwa siku moja maeneo ya Apollo yatavutia watalii ambao wataweza kuchukua vumbi la mwezini ambalo linakata kama majani na linaloweza kjuwa hatari.

Advertisement