Trump akubali mwaliko wa Malkia Elizabeth
Muktasari:
- Rais wa Marekani Donald Trump ataanza ziara nchini Uingereza Juni 3 mpaka 5 na ataongozana na mke wake Melania
Washington,Marekani.Rais wa Marekani, Donald Trump atazuru Uingereza mapema Juni kwa mwaliko rasmi wa Malkia Elizabeth II.
Taarifa iliyotolewa leo na Ikulu ya Washington, imeeleza kwamba, Trump na mkewe Melania wameukubali mwaliko huo wa Malkia na kwamba watafanya ziara hiyo Juni 3 had 5.
Taarifa hiyo inaeleza kwamba, Trump na mkewe watahudhuria maadhimisho ya mika 75 ya uvamizi uliofanywa na muungano wa kijeshi dhidi ya wapiganaji wa ki-Nazi, maarufu D-Day, ulioleta ushindi wa muungano huo wakati wa vita vya pili vya dunia.
Ikulu ya Marekani ilieleza kwamba baada ya ziara hiyo ya kitaifa, Trump na ujumbe wake wataendelea na ziara nchini Ufaransa ambako watakutana na Rais Emmanuel Macron.
Trump na Melania walikutana na Malkia kwa muda mfupi katika kasri la Windsor, wakati wa ziara ya rais huyo nchini Uingereza iliyofanyika Julai mwaka uliopita.