Uingereza yapiga marufuku ndege za Boeing 737 Max kupita kwenye anga yake

Tuesday March 12 2019

 

London,Uingereza. Uingereza na Shirika la ndege la Singapore wamesitisha wamepiga marufuku ndege za Boeing 737 Max  kupita kwenye anga zake.

Uamuzi huo umetolewa baada ya ndege ya kampuni ya ndege ya Ethiopia aina ya Boeing Max 8 kuanguka Jumapili, na kuwauwa watu 157 waliokuwemo.

Ilikuwa ni ajali ya pili iliyohusisha ndege ya aina hiyo katika kipindi cha chini ya miezi mitano iliyopita.

Uwanja wa Changi nchini Singapore ni wa tano wenye kuwa na shughuli nyingi zaidi duniani na kiituo kinachounganisha safari nyingi za kutoka bara Asia hadi Ulaya na Marekani.

Ndege hiyo ya ya shirika la ndege la Ethiopia ilianguka saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki  ikiwa na abiria 149 pamoja na wafanyakazi 8.

Msemaji wa shirika hilo ambaye hakutowa jina lake  alithibitisha  juu ya taarifa hiyo ambapo imetajwa ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Nairobi nchini Kenya.

Advertisement