Viongozi wa upinzani Sudan waachiwa huru

Monday June 10 2019

Khartoum Sudan. Jeshi la Sudan limewaachia huru viongozi wenye ushawishi wa vuguvugu la maandamano nchini humo.

Viongozi hao watatu wa upinzani walikamatwa wiki iliyopita ikiwa ni siku moja baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dk Abily Ahamed.

Kwa siku mbili mfulululizo wananchi nchini humo wanafanya maandamano kushinikiza jeshi la nchi hiyo kukabidhi madaraka kwa Serikali ya kiraia.

Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na Serikali ya Sudan kimeripoti leo Jumatatu June 10, kuwa viongozi hao Yasir Arman ambaye ni naibu mkuu wa vuguvugu hilo,Ismail Jalab na Mubarak Ardol wamechiwa huru ingawa haukufahamika mara moja wameachiwa lini.

Inadaiwa Arman alikamatwa Juni 5, siku mbili baada ya watu waliovalia magwanda ya kijeshi kuvunja maandamano ya wiki kadhaa nje ya makao makuu ya jeshi la Sudan mjini Khartoum na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100 wakati Jalab na Ardol walizuiliwa katika makazi yao.

Advertisement