Walioathiriwa na vita kuishtaki Serikali Kenya

Saturday April 20 2019

Nairobi,Kenya. Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya, wanaazimia kuishitaki Serikali na asasi zake wakiwemo polisi kutokana na dhulma walizofanyiwa wakati wa ghasia hizo.

Mashirika ya kijamii nchini Kenya yanaazimia kuishtaki, serikali na asasi zake wakiwemo viongozi wa  polisi, kwa niaba ya waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya.

Kesi hiyo itakuwa ni kufanyiwa vitendo vibaya katika kipindi cha uchaguzi hasa baada ya kutangazwa matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa kituo cha kijamii cha Kondele kinachojishugulisha na masuala  ya haki za binadamu  Bonface Ogutu Akach anasema wameshirikiana na mashirika kadhaa kuwapa fursa waathiriwa wa ghasia hizo kutoka Migori, Siaya, Homabay na Kisumu kudai haki na fidia Serikalini.

Alisema wakati huo wananchi wengi walifanyiwa vitendo viouvu ikiwamo kubakwa kujeruhiwa na kupoteza mali zao.

 

Advertisement

 

Ofisa wa shirika la Kiislamu la haki za binadamu, MUHURI, Francis Auma amesema lengo la kuwaleta pamoja waathiriwa hao ni kukusanya ushahidi wa kutosha kuweza kuishtaki Serikali.

Advertisement