Wanasiasa 3000 wakutana Uswis

Wednesday January 23 2019

Davos,Uswis. Zaidi ya  wanasiasa 3,000 na wakurugenzi  duniani wanaanza leo mkutano wao wa kila mwaka katika eneo la kitalii la Davos nchini Uswisi, kujadili ufumbuzi wa changamoto za kimataifa licha ya kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi muhimu duniani.

Rais mpya wa Brazil wa siasa kali za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro atatoa hotuba ya kwanza kuu katika mkutano huo wa siku nne wa Jukwaa la Dunia la Kiuchumi.

Rais huyo wa Brazil anachukua nafasi ya Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alifuta ziara yake ili kushughulikia hali inayoendelea nchini mwake ya kusitishwa kwa baadhi ya shughuli za Serikali.

Advertisement