Watafiti wabaini binadamu mwingine wa kwanza

Ugiriki. Watafiti wamebaini kuwapo aina ya binadamu wa kwanza anayefanana na binadamu aliyeishi miaka 210,000 iliyopita.

Fuvu lililofukuliwa nchini Ugiriki limegunduliwa mtu huyu aliishi wakati ambapo Ulaya ilichukua aina ya kizazi cha binadamu kilichojulikana kama Neanderthali, imeripoti BBC.

Matokeo ya uvumbuzi huu yamechapishwa katika jarida la masuala asili.

Watafiti walifichua mafuvu ya binadamu hao kwenye pango la Apidima nchini Ugiriki katika miaka ya 1970.

Moja ya mafuvu hayo lilikuwa limeharibika lakini jingine lilikuwa kamili, na ilibidi utumiwe mtambo wa kompyuta kuchunguza na vipimo kadhaa vya uranium vinavyobashiri tarehe, ili kufichua taarifa kuhusu mafuvu hayo.

Fuvu lililokuwa kamili lilionekana kuwa ni la aina ya binadamu wa Neanderthali. Lakini jingine lilionyesha tabia wazi, kama vile muundo wa duara kwenye sehemu ya nyuma ya fuvu, ambalo ni sawa na lile tulilonalo binadamu wa sasa.

Vilevile fuvu la Neanderthali lilikuwa ni la mtu aliyekuwa na umri mdogo.

“Tulichokishuhudia ni kwamba nchini Ugiriki walikuwapo watu wa kizazi cha binadamu kinachofanana na cha sasa kariobu miaka 210,000 iliyopita, chenye idadi ambayo labda inaweza kulinganishwa na watu wa Levant, lakini nafasi yao ikachukuliwa na binadamu wa aina ya Neanderthali yapata miaka 170,000 iliyopita," amesema Profesa Chris Stringer, mtafiti mwenza, kutoka katika kituo cha makumbusho ya historia ya masuala ya asili mjini London.

Huku binadamu wa sasa wakiishi katika maeneo ya Ulaya na Asia, wamechukua kwa kiasi kikubwa nafasi ya jamii za binadamu wengine kama vile Neanderthali na Denisovani.

Lakini huu haukuwa uhamiaji wa kwanza wa binadamu wa kisasa (Homosapiens) kutoka Afrika.

Mafuvu ya Homo sapieni kutoka maeneo ya Skhul na Qafzeh nchini Israel yaliyobainika miaka ya 1990 yaliiishi kati ya miaka 90,000 na 125,000 iliyopita.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, imekuja kutambuliwa kuwa vizazi vya binadamu wa kale viko nje ya Afrika mapema hata zaidi ya ilivyoaminiwa awali.

Katika miaka michache iliyopita, wataalam wa uvumbuzi wa muundo na mabadiliko ya mafuvu ya binadamu kutoka Daoxian na Zhirendong nchini Uchina walisema mafuvu hayo ni ya binadamu walioishi kati ya 80,000 na 120,000 iliyopita.

Uchunguzi wa DNA ulibaini ishara za mchanganyiko wa vizazi vya binadamu wa Afrika na Neanderthali. Ushahidi kutoka wa binadamu wa kizazi cha Ujerumani cha Neanderthali unaonyesha kuwa mchanganyiko huo ulitokea baina ya miaka 219,000 na 460,000 , ingawa haijabainika wazi ikiwa kizazi cha binadamu wa kale cha Homo sapieni kilihusika, au kikundi kingine cha Waafrika wa kale.