Watu 10 wauawa DRC kufuatia shambulizi la ADF

Wednesday January 9 2019

Beni, DRC. Watu  wanane  wameuwawa  ikiwa  ni  pamoja  na  wanne ambao  ni  ndugu  wa  wanajeshi, katika  wilaya  ya  Mavivi Kaskazini  mwa  eneo  la  Beni, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Msemaji  wa  jeshi  wa jimbo  hilo  Mark Hazukay  ameliambia  shirika  la  habari  la Ufaransa  AFP kuwa polisi wametaja idadi ya waliouwawa  kuwa  ni  10  kabla ya  kutangaza tena kuwa  waliouwawa  ni  wanane.

Raia 10  wameuawa Mashariki mwa DRC kufuatia shambulizi linalodaiwa kufanywa na kundi la ADF.

Kwa mujibu wa Hazukay, watu hao  wameuawa wakiwamo ndugu wa wanajeshi, katika  wilaya  ya  Mavivi Kaskazini mwa eneo la Beni.

Advertisement