Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru agoma kuzindua mradi Dodoma.

Wednesday August 14 2019

 

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mradi wa kiwanda cha kuchakata zabibu unaomilikiwa na Chama cha Wakulima wa Zabibu na Masoko Mpunguzi umeshindwa kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kubainika kutofuata taratibu za Serikali.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Mkongea Ali amegoma kufanya hivyo leo Agosti 14 mwaka 2019 baada ya kuukagua na kubaini kuwa kuna taratibu zimekiukwa, wakati wa tukio hilo alikuwepo Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu  Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde  ambaye ni Mbunge wa Dodoma.

Pia, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mradi huo na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi makao makuu ya Takukuru na kwake, baada ya wiki mbili.

Taratibu hizo zinazodaiwa kukiukwa ni kukosa leseni ya biashara, kutokuwa na mashine ya kielektroniki na kukosa cheti cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

"Baada ya kuukagua nimebaini kuwa kuna taratibu zimekiukwa. Kiwanda kinaingiza Sh520milioni inawezekana kuna watu wanapita chini kwa chini na kukusanya kodi na fedha zinaishia mikononi mwa watu bila Serikali kupata mapato yake," amesema.

Advertisement